Jumamosi, 11 Juni 2016

MUHAMED ALI AZIKWA

Bingwa wa zamani wa masumbwi duniani alizikwa siku ya Ijumaa ya tarehe 10 Juni, 2016 ambapo msafara wa magari maalum 17 uliongozana eneo la Kentucky kuelekea nyunmbani kwao Louisville kwa mazishi ambapo mamia ya watu walijipanga kando ya barabara wakirusha maua kwenye gari iliobeba mwili wa bondia huyo wakipiga kelele za kutaja jina lake, Ali! Ali! Ali! kama ishara ya kumuaga shujaa huyo wa ngumi. Watu mbalimbali mashuhuri walihuzulia wakiongozwa na rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton.  MUNGU ailaze roho ya Ali pema. AMIIM.

Alhamisi, 9 Juni 2016

LUNINGA YA ZBC NDIO LUNINGA KONGWE YA RANGI BARANI AFRIKA

Abeid Karume 1964.jpgKituo cha Luninga cha taifa cha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ndio kituo cha mwanzo kurusha matangazo ya picha za rangi mnamo miaka ya 1970. Chini ya Rais wa kwanza hayati Abeid Amani Karume Zanzibar iliweza kujenga na kufungu kituo hicho ambacho mpaka sasa kinatoa huduma ya matangazo kwa wigo mpana zaidi bara na visiwa kwana la ZBC TV zamani TVZ ambapo jengo lake lilipewa jina la KARUME HOUSE kwa heshima ya Raisi huyo wa kwanza wa visiwa hivi vya Zanzibar. 

KUMBE BINADAMU WA KALE ALIISHI TANZANIA

Nyayo za mtu wa kale zilizogunduliwa eneo la bonde la ufa eneo la Ngorongoro mkoa Arusha pamoja na fuvu la binadamu wa kale imekuwa ni uthibitisho wa kuamini kuwa wapo binadamu wa kale kabla yetu waliishi katika eneo hilo

SITI BINT SAAD MWANAMKE WA KWANZA AFRIKA KURIKODI NYIMBO ZAKE KWENYE SANTULI


Image result for siti binti saad "Unguja njema atakae aje" ni msemo aliousema Siti bint Saad mzaliwa wa kijiji cha Fumba mjini Unguja mwaka 1880. Alijaliwa kipaji cha sauti nyororo na muumba hali iliopelea kuwa mtoa burudani ya kuimba maulana sultan wa Zanzibar na kufanikiwa kwa mara ya kwanza kwanda ughaibuni huko India mwanzoni katikati mwa miaka ya 1920 na kurikodi nyimbo zake nyingi zilizompatia sifa nyingi yeye na kisiwa cha Unguja kwa ujumla, miongoni mwa nyimbo hizo ni Wewe paka, Muhogo wa Jang'ombe, Kijiti na nyenginezo.

ALIYEWAHI KUWA DIKTETA AKIWA NA UMRI MDOGO KULIKO MADIKTETA WATE DUNIANI

Image result for francisco franco   Katika historia ya madikteta duniani wengi humtaja Adolf Hetler wa Ujerumani na Augasto Pinochet wa Chile, lakini lipo jina la Francisco Franco aliyekuwa dikteta wa Hispania kuanzia 1939 hadi 1973 akiwa na  miaka 47ikiwa ni umri mdogo zaidi ukilinganisha na umri wa madikteta wangine watatu waliotikisa dunia akiwemo na Miguel Primo De Rivera wa huko huko Hispania. Hakutambulika sana ila alipata umaarufu kwa kitendo chake cha kukataa kuunganisha majeshi yake na yale ya NAZI katika harakati za Hitler kuitawala dunia.

UNAJUA MWANZO WA KUTUMIANA KADI?

The First Christmas CardInaaminika Bwana Herny Cole ndie mbunifu wa kadi kwenye msimu wa Krismas ya mwaka 1840 huko Uingereza. Baada ya kuitangaza na watu kuelewa ilianza kutumika rasmi mwaka 1843 ambapo iliuzwa kwa thamani  ya shilingi 1. Tangu hapo utamaduni huu uliendelea na kushika kasi hadi leo watu hutumia kadi kama sehemu ya mualiko wa harusi, maulidi na hata mazishi ya watu mashuhuri.

KUMBE MUZIKI NI SILAHA!!!!

NoneMuziki sio burudani kama ilivyozoeleka, lakini unaweza kuwa hatari kuliko bunduki. Hili linaweza kuthibitishwa na tukio lililotokea nchini Kenya mwanzoni mwa miaka ya 50 pale lilipoundwa kundi la harakati za ukombozi lililojulikana kama "Maumau" ambalo liliibuka baada ya kundi la muziki la "FRANK NA DADA ZAKE" la nchini Tanzania wakati huo Tanganyika lilipotunga wimbo ulioitwa "YES NO KIZUNGU SIKIJUI" ambao ulikuwa ukihamasisha watu kuuchukia ukoloni kwa nguvu zao zote, wimbo huo ulipigwa marufuku na utawala wa kikoloni wa kiingereza wakati huo sababu ulihamasisha ukoloni kupingwa kona zote za Afrika Mashariki.